Posts

Showing posts from April, 2023

71 - Kesheni Kaombeni

71 - Kesheni Kaombeni "Watch , For THe Time Is Short" 1. Kesha ukaombe panapo mafasi;  Wakati si mwingi. Kwa vile ukeshe  Mwili ni dhaifu. Adui hodari  karibu atakuja, Bwana wa arusi.  Kesha, Omba, Kesha, Omba, Kesha Kaombe gizani, mchana, Daima kesha.  2. Fukuza usingizi, fukuza mashaka;  Ahadi ni yako, raha ya milele  Bwana alkesha kwa ajili yako; Jasho yeke ikawa matone ya dame.  3. Yesu umkubali awe nguvu zako;  Silaha uzivae; adui karibu.  Sasa nafasi iko, isipite bure;  Bila kukawia masihiya kesha. ( Amina)

72 - Jenga Juu Ya Mwamba

72 - Jenga Juu Ya Mwamba 1. Tuta jenga juu ya Mwamba Wa Yesu, Mwaba wa kale; Tutavumilia kishindo Tufani ivumapo. Tuta jenga juu, ( tutajenga juu ya Mwamba mkuu) Tuta jenga juu, ( tutajenga juu ya Mwamba mkuu) Tutajenga juu ya Mwamba mkuu, Juu yake yesu. 2. Wengine hujenga katika Mchanga wa ulimwengu; Wengine katika mawimbi Ya anasa za dhambi. 3. Jenga nawe juu ya mwamba, Msingi pekee wa kweli: Tumai lake litadumu, Tumai la wokovu.   ( Amina)

73 - Bwana, Uniongoze Juu

73 - Bwana, Uniongoze Juu      "Higher Ground" 1. Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu; Naomba nikisafiri, "Bwana uniongoze juu." Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu. Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze juu. 2. Moyo wangu hautaki Kukaa palipo shaka; Wengine wapenda chini Nia yangu ni kupanda. 3. Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui; Kwa imani nasikia Sauti ya washindaji. 4. Kupanda juu nataka Niuone utukufu; Hata mwisho nitaomba, "Bwana uniongoze juu."   ( Amina)

74 - Niambie, Ee Mlinzi

74 - Niambie, Ee Mlinzi "Watchman, Tell Us Of The Night" 1. Niambie, Ee mlinzi, Umepambazuka je! Utukufu wa Zayini, Pana dalili zake? Msafiri uondoke, Utazame mbinguni, Kiunoni ujifunge, Ni kucha alfajiri. 2. Mlinzi inamulika Nuru njiani mwako, Dalili za kuja kwake, Kwamba siku karibu; Panda itakapolia Itawaamsha wafu, Watakatifu wa Mungu, Kuwapa kutokufa. 3. Mlinzi, ione nuru Ya mwaka wa Sabato; Sauti zinatangaza Ufalme ni karibu; Msafiri ninaona Mlima wa Zayuni, Mji wa Yerusalemi Nayo fahari yake. 4. Kwenye mji wa dhahabu Anaketi mfalme Katika kiti kizuri: huku anatawala. Pana amani po pote, Mashamba husitawi; Na ardhi ina rutuba; Mito ni mitulivu. 5. Mlinzi, twaribia Nchi iliyo nzuri; Twende mbele, tufurahi, Nchi inachangamka, Sikieni kuna wimbo Wa waliookoka; Kaza mwendo, Ujiunge Na kundi Kubwa hili.   ( Amina)

75 - Msini Imara, Ninyi Wa Bwana

75 - Msini Imara, Ninyi Wa Bwana "How Firm A Foundation" 1. Msingi imara, ninyi wa Bwana, Umewekwa kwenu kwa neno lake. Nini zaidi atasema Bwana,  Imaniyenu ipate kuzidi? 2. Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka haitazidi; `Takuwapo nawe, nikuwezeshe, Shida upatazo zisikutishe! 3. Utakapopishwa ndani ya moto Nguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako. Nazitasalia dhambi zako. 4. Na mtu aliye nitegemea Nguvu za Jehanamu zijapotisha, Kamwe kwa adui sitamtia; Mtu wangu kamwe sitamwacha.   ( Amina)

76 - Mrithi Ufalme

76 - Mrithi Ufalme "Heir Of The Kingdom" 1. Mrithi ufalme, kwani walala? Karibu wokovu wasinzia? Amka, simama, uvae silaha,  Haraka sana, saa zapita. 2. Mrithi ufalme mbona `kawia?  M-bona hupokei zawadi? Haya, uvae, Mwokoziyuaja;  Haraka, umlaki afikapo. 3. Mataifa makuu ya dunia!  Yapigana kujiangusha; Usisihofu dalili, mrithi;  Ishara zote hazikawii. 4. `Sitazame anasa za dunia, Kwani hayo yapita upesi; Zivunje kamba zinazokufunga; Mrithi ufalme, njoo` karudi. 5. Inua kichwa, tazama mbele tu, M-falme aja na utukufu; Jua laonekana milimani, Warithi ufalme furahini.   ( Amina)

77 - Habari Za Usiku

77 - Habari Za Usiku "Watchmen On The Walls Of Zion" 1. Je! Mkinzi ukutani  Wa mji wa Zayuni,  Habari zake usiku?  Asubuhi karibu?  Kuna dalili za kupambazuka?  Kuna dalili za kupambazuka?  2. Katika safari yetu  Twaona nchi kavu?  Tutalala baharini?  Bandari bado mbali?  Kweli, kweli tutaona ufalme?  Kweli, kweli tutaona ufalme?  3. Tunaona nuru yake  Nyota ya asubuhi;  Nyota, tukufu na safi  Inang`aa mbinguni;  Furahini, wokovu u karibu.  Furahini, wokovu u karibu.  4. Tumetazama ramani,  Kweli pwani si mbali;  Twende mbele, kwa upesi  Tutaona bandari;  Furahini, imbeni nyimbo zenu, Furahini, imbeni nyimbo zenu.   ( Amina)

78 - Mpaka Lini Bwana

78 - Mpaka Lini Bwana "How Long, O Long Our Saviour" 1. Mpaka lini Bwana, Utakaa mbali? Kumetuchosha moyo kukawia hivi. Utatujia lini, Ili tufurahi Katika ile nuru, kuja kutukufu? 2. Mpaka lini Yesu, Utaacha watu Uliowakomboa, Wawe na mashaka? Wachache waamini, Kwamba utarudi; Wachache wa tayari, Bwana kukulaki. 3. Waamshe watu wako, Tangaza kilio: "Mwe watakatifu, Bwanayu karibu!" Utatujia lini, Ili tufurahi Katika ile nuru, Kutukufu? ( Amina)

79 - Nataka Imani Hii

79 - Nataka Imani Hii "O For A Faith" 1. Nataka Imani hii: Imani imara, Ambayo haitetemi Kitu chote  Wakati wa shida,  Wakati wa shida.  2. Isiyonung`unika Huzuni, taabu;  Lakini katika saa ya matata  Humwamini Mungu,  Humwamini Mungu.  3. Imani inayo ng`aa katika tufani;  Isiyoogopa giza, wala shida,  Njaa na Hatari,  Njaa na hatari.  4. Haiogopi dunia, Kudharau kwake;  Haiangushwi na hila, na uwongo  Dhambi na ogofyo,  Dhambi na ogofyo.  5. Bwana, nipe imani hii, Hivi nitaweza  Kuonja hapa chini ulimwenguni,  Kurithi furaha,  Kurithi furaha.  ( Amina)

80 - Tupe Moto Wa Injili

80 - Tupe Moto Wa Injili "O For That Flame Of Living Fire' 1. Tupe moto wa uhai Uliowaka zamani,  Uliowaongoza juu Wazee watakatifu.  2. Wapi roho iliyokaa Moyoni mwa Ibrahimu?  Kadhalika ndugu Paulo Aliwezeshwa na moto.  3. Neema yako haina Nguvu siku hizi sawa  Kama wakati wa Musa, Ayubu na wa Eliya?  4. Zamani za kale, Bwana, Kumbuka na kwa rehema,  Zihuishe roho zetu Kwa Roho Mtakatifu.   ( Amina)

81 - Siku Sita Zimepita

81 - Siku Sita Zimepita "Another Six Days' Work" 1. Siku sita zimepita, Sabato tena karudi;  Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.  2. Msifuni awapaye pumziko tamu wachovu,  Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.  3. Moyo wetu ufurahi, na kutoa mashukuru;  Ujalizwe raha ile, yasipitikwa kamwe.  4. Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko  Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko. ( Amina)

82 - Ni Siku Ya Furaha

82 - Ni Siku Ya Furaha "O Day Of Rest And Gladness" 1. Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;  Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;  Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,  Hukaribia mbingu, lilipo baraka.  2. Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,  Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:  Kijito cha baridi kimefanya ziwa,  Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.  3. Leo ngazi na iwe ifakayo juu,  Mawazo na yasiwe ya duniani tu;  Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,  Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.   ( Amina)

83 - Ewe Skuli Ya Sabato

83 - Ewe Skuli Ya Sabato "Sweet Sabbath School" 1. Ewe skuli ya Sabato,  U pazuri sana;  Moyo wangu wanivuta,  Nije kwako leo.  Sabato . . . ni nzuri . . .  Sabato . . . ni nzuri . . .  Moyo wangu wanivuta,  Nije kwako leo.  2. Moyo wangu mpotovu,  Hapa una raha;  Ndipo nimwonapo Yesu,  Nije kwako leo.  3. Hapa Yesu mwenye pendo  Aniita pole:  Nimtolee moyo Yeye,  Nije kwako leo.  ( Amina)

84 - Ikumbuke Sabato

84 - Ikumbuke Sabato 1. Ikumbuke kote Sabato ya Bwana,  Siku tamu na bora, kupita nyingine;  Yatuletea raha, na furaha kweli,  Mwanga wake hungaza, urembo wa Yesu.  Karibie, karibie, Sabato tamu;  Karibie, Yesu pia, Bwana wa raha.   2. Itakase kweli, ukamsifu leo,  Yeye aliye sema "Mimi ndiye njia";  Nasi tukimfuata mkombozi hapa.  Atatunywesha tele maji ya uzima.  3. Siku ya nderemo! Tupishe wakati,  Tukimwimbia Yesu Rafiki Mpendwa;  Mponya wetu leo, U mwema ajabu!  Ukae kwetu, Bwana, moyoni daima.   ( Amina)

85 - Salama Tumepita

85 - Salama Tumepita "Safely Through Another Week" 1. Salama tumepita, safarini juma hii,  Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa:  Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma;  Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.  2. Utupe nuru leo toka hazina yako;  Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo;  Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,  Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.  3. Twakusanyika hapa, tusifu jina lako;  Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana;  Utamu tusikize, wa raha ya milele:  Utamu tusikize, wa raha ya milele:  4. Injili yako leo, ishike wenye dhambi;  Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida;  Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,  Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.    ( Amina) 

86 - Ukaribie Tena

86 - Ukaribie Tena "Welcome, Welcome, Day Of Rest" 1. Ukaribie tena, ewe siku ya raha;  Roho yakusalimu kama mwanga wa mbingu.  2. Raha yako tulivu, yafurahisha moyo;  Yatuliza taabu, hata waisha mwendo.  3. Ee siku takatifu, sifa na maombi,  Na kutuhekimisha, baraka yako kubwa.   ( Amina) 

87 - Siku Ya Sabato

87 - Siku Ya Sabato "Thy Holy Sabbath Lord" 1. Siku ya Sabato, siku takatifu,  Watu wako Mungu wetu, waipenda sana.  2. Ulitakasa, uliibariki,  Siku hiyo ya Sabato, siku yako Bwana.  3. Nasi tubariki tukikuabudu,  Katika siku ya raha, siku yako Bwana.  4. Halafu mbinguni, pamoja na Wewe.  Tunataka kuzishika Sabato za Bwana.  ( Amina) 

88 - Siku Hii Ya Sabato

88 - Siku Hii Ya Sabato "How Sweet Upon This Sacred Day" 1. Siku hii ya Sabato, Tamu kufikiri  Juu ya Mungu na Mbingu Kuacha dunia.  2. Tamu kusikia Neno Toka mhubiri  Anayefundisha toba, Tupate uzima.  3. Katika vita na dhambi, Ikiwa twashindwa,  Yeye atatupa nguvu Aonaye moyo. ( Amina) 

89 - Asubuhi

89 - Asubuhi "Lord, In The Morning" 1. Bwana asubuhi kucha nitakuinua  Sauti yangu kuomba, nipate baraka.  2. Nakuomba roho yako niongozwe nayo;  Nifanye yanipasayo, na mapenzi yako.  3. Wanaokutegemea, U Mlinzi wao;  Matumaini wanayo, utayatimiza.  4. Na kwa wingi wa fadhili, Nyumbani mwako juu  Nitaingia na wimbo, Pale kusujudu.  (Amina) 

90 - Mapya Ni Mapenzi

90 - Mapya Ni Mapenzi "New Every Morning" 1. Mapya ni mapenzi hayo,  Asubuhi tuonayo;  Saa za giza hulindwa,  Kwa uzima kuamka.  2. Kila saku, mapya pia,  Rehema, wema na afya,  Wokovu na msamaha,  Mawazo mema, furaha.  3. Tukijitahidi leo  Na mwendo utupasao,  Mungu atatueleza  Yatakayompendeza.  4. Mamboyetu ya dunia  Bwana atayang'aria,  Matata atageuza  Yawe kwetu ya baraka.  5. Yaliyo madogo, haya  Bwana tukimfanyia,  Yatosha: tutafaidi  Huvuta kwake zaidi.  6. Ewe Bwana, siku zote,  Tusaidie kwa yote:  Mwendo wetu wote vivyo,  Uwe kama tuombavyo.   (Amina) 

91 - Kaa Nami

91 - Kaa Nami "Abide With Me" 1. Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu kaa nami. 2. Siku zetu hazikawi kwisha; Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi; Usiye na mwiso, kaa nami. 3. Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe Bwana, kaa nami. 4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako kaa nami. 5. Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za mbinguni hazikomi; Siku zangu zote kaa nami. (Amina) 

92 - Magharibi Jua

92 - Magharibi Jua "Day Is Dying In The West" 1. Magharibi jua limekwisha kushuka, Mwezi na nyota sasa vinamsifu Muumba wa usiku Mungu Mtukufu, Mungu Mkuu, Wote juu mbinguni, na wanadamu chini Twakusifu. 2. Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni. Utuifadhi sisi, tufahamu gizani, U karibu. 3. Mapenzi yako makuu yawe nasi usiku, Tuli usingizini, kucha vivyorohoni tushukuru. 4. Na utakapo kuja na nguvu kutawala, Mungu wangu kubali kunichukua mimiulko juu. Baba, Mwana, Roho, Mungu wetu, Wote juu mbinguni, na wanadamu chini twakusifu. (Amina) 

93 - Jua La Rohoni Mwangu

93 - Jua La Rohoni Mwangu "Sun Of My Soul" 1. Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu; Usiku  giza hapana, ukiwa karibu Bwana 2. Nikipata usingizi, nijaze fikira hizi, Nitamu sana, nilale pendoni mwako milele. 3. Kaa nami, ewe Bwana, usiku kama mchana, Nisiishi mbali nawe; ni uhai kuwa nawe. 4. Kama mtotomnyonge ameshawishwa atange, Mtafute Ewe Bwana, ujirudishie tena. 5. Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini, Waliao, Mtulizi, wape wote usingizi. 6. Asubuhi tutokapo, tukaribie tulipo; Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.   (Amina)

94 - Po Pote Mashamba Yajaa

  94 - Po Pote Mashamba Yajaa "Far And Near The Fields" 1. Popote mashamba yajaa tele nafaka pevu,  Popote yang`aa meupe bondeni na nyandani. Mwenye mavuno twasihi upeleke wavuni, Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe. 2. Wapeleke uchaoni, waende na jotoni, Hata jua lishukapo wakusanye ko kote. 3. Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao, Na jioni ingieni kwake na furaha kuu. (Amina)

95 - Zileteni Zaka Kwa Hazina

95 - Zileteni Zaka Kwa Hazina "Hear The Words Of Scripture" 1. Sikieni neno la Mungu wetu, zileteni zaka kwa hazina Leteni na mioyo yenu yote; mibaraka itakuja. Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo; Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafasi ya kupewa. 2. Wakati Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utabarikiwa. 3. Je,una kasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina, Uzilete kama alivyo sema, Ndipo utabarikiwa. 4. Ushukuru Bwana na moyo wote, unapo leta zaka ghalani; Usadiki ahadi zake zote, ndipo utabarikiwa. 5. Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta  zaka ghalani Twimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.   (Amina)