Posts

71 - Kesheni Kaombeni

71 - Kesheni Kaombeni "Watch , For THe Time Is Short" 1. Kesha ukaombe panapo mafasi;  Wakati si mwingi. Kwa vile ukeshe  Mwili ni dhaifu. Adui hodari  karibu atakuja, Bwana wa arusi.  Kesha, Omba, Kesha, Omba, Kesha Kaombe gizani, mchana, Daima kesha.  2. Fukuza usingizi, fukuza mashaka;  Ahadi ni yako, raha ya milele  Bwana alkesha kwa ajili yako; Jasho yeke ikawa matone ya dame.  3. Yesu umkubali awe nguvu zako;  Silaha uzivae; adui karibu.  Sasa nafasi iko, isipite bure;  Bila kukawia masihiya kesha. ( Amina)

72 - Jenga Juu Ya Mwamba

72 - Jenga Juu Ya Mwamba 1. Tuta jenga juu ya Mwamba Wa Yesu, Mwaba wa kale; Tutavumilia kishindo Tufani ivumapo. Tuta jenga juu, ( tutajenga juu ya Mwamba mkuu) Tuta jenga juu, ( tutajenga juu ya Mwamba mkuu) Tutajenga juu ya Mwamba mkuu, Juu yake yesu. 2. Wengine hujenga katika Mchanga wa ulimwengu; Wengine katika mawimbi Ya anasa za dhambi. 3. Jenga nawe juu ya mwamba, Msingi pekee wa kweli: Tumai lake litadumu, Tumai la wokovu.   ( Amina)

73 - Bwana, Uniongoze Juu

73 - Bwana, Uniongoze Juu      "Higher Ground" 1. Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu; Naomba nikisafiri, "Bwana uniongoze juu." Bwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu. Juu kuliko dunia; Bwana uniongoze juu. 2. Moyo wangu hautaki Kukaa palipo shaka; Wengine wapenda chini Nia yangu ni kupanda. 3. Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui; Kwa imani nasikia Sauti ya washindaji. 4. Kupanda juu nataka Niuone utukufu; Hata mwisho nitaomba, "Bwana uniongoze juu."   ( Amina)

74 - Niambie, Ee Mlinzi

74 - Niambie, Ee Mlinzi "Watchman, Tell Us Of The Night" 1. Niambie, Ee mlinzi, Umepambazuka je! Utukufu wa Zayini, Pana dalili zake? Msafiri uondoke, Utazame mbinguni, Kiunoni ujifunge, Ni kucha alfajiri. 2. Mlinzi inamulika Nuru njiani mwako, Dalili za kuja kwake, Kwamba siku karibu; Panda itakapolia Itawaamsha wafu, Watakatifu wa Mungu, Kuwapa kutokufa. 3. Mlinzi, ione nuru Ya mwaka wa Sabato; Sauti zinatangaza Ufalme ni karibu; Msafiri ninaona Mlima wa Zayuni, Mji wa Yerusalemi Nayo fahari yake. 4. Kwenye mji wa dhahabu Anaketi mfalme Katika kiti kizuri: huku anatawala. Pana amani po pote, Mashamba husitawi; Na ardhi ina rutuba; Mito ni mitulivu. 5. Mlinzi, twaribia Nchi iliyo nzuri; Twende mbele, tufurahi, Nchi inachangamka, Sikieni kuna wimbo Wa waliookoka; Kaza mwendo, Ujiunge Na kundi Kubwa hili.   ( Amina)

75 - Msini Imara, Ninyi Wa Bwana

75 - Msini Imara, Ninyi Wa Bwana "How Firm A Foundation" 1. Msingi imara, ninyi wa Bwana, Umewekwa kwenu kwa neno lake. Nini zaidi atasema Bwana,  Imaniyenu ipate kuzidi? 2. Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka haitazidi; `Takuwapo nawe, nikuwezeshe, Shida upatazo zisikutishe! 3. Utakapopishwa ndani ya moto Nguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako. Nazitasalia dhambi zako. 4. Na mtu aliye nitegemea Nguvu za Jehanamu zijapotisha, Kamwe kwa adui sitamtia; Mtu wangu kamwe sitamwacha.   ( Amina)

76 - Mrithi Ufalme

76 - Mrithi Ufalme "Heir Of The Kingdom" 1. Mrithi ufalme, kwani walala? Karibu wokovu wasinzia? Amka, simama, uvae silaha,  Haraka sana, saa zapita. 2. Mrithi ufalme mbona `kawia?  M-bona hupokei zawadi? Haya, uvae, Mwokoziyuaja;  Haraka, umlaki afikapo. 3. Mataifa makuu ya dunia!  Yapigana kujiangusha; Usisihofu dalili, mrithi;  Ishara zote hazikawii. 4. `Sitazame anasa za dunia, Kwani hayo yapita upesi; Zivunje kamba zinazokufunga; Mrithi ufalme, njoo` karudi. 5. Inua kichwa, tazama mbele tu, M-falme aja na utukufu; Jua laonekana milimani, Warithi ufalme furahini.   ( Amina)

77 - Habari Za Usiku

77 - Habari Za Usiku "Watchmen On The Walls Of Zion" 1. Je! Mkinzi ukutani  Wa mji wa Zayuni,  Habari zake usiku?  Asubuhi karibu?  Kuna dalili za kupambazuka?  Kuna dalili za kupambazuka?  2. Katika safari yetu  Twaona nchi kavu?  Tutalala baharini?  Bandari bado mbali?  Kweli, kweli tutaona ufalme?  Kweli, kweli tutaona ufalme?  3. Tunaona nuru yake  Nyota ya asubuhi;  Nyota, tukufu na safi  Inang`aa mbinguni;  Furahini, wokovu u karibu.  Furahini, wokovu u karibu.  4. Tumetazama ramani,  Kweli pwani si mbali;  Twende mbele, kwa upesi  Tutaona bandari;  Furahini, imbeni nyimbo zenu, Furahini, imbeni nyimbo zenu.   ( Amina)